Na Asha Shaban,Tarime.
Idadi ya watoto wasio jua kusoma na kuandika wa darasa la
kwanza mpaka la tatu katika Halmashauri ya Tarime mjini mkoani mara
imepungua kutoka watoto 3268 mwaka 2015 hadi watoto 2628
mwaka 2017 kutokana
na kuwepo na vituo vya utayari
vilivyopo chini ya mpango
wakuboresha elimu Nchini Tanzania(EQUIP).
Akizungumza na wandishi wa habari walio tembelea Mradi huo
hivi karibuni Afisa Elimu Msingi Daniel Makorere alisema kuwa idadi ya watoto imeongezeka katika uandikishwaji kutoka
watoto 9809mwaka 2015 hadi watoto 14,104 mwaka huu.
Aliongeza kuwa vituo
hivyo vya utayari vilianzishwa mahususi kutokana na watoto wengi kuanza darasa
la kwanza kwa kutokuwa na msingi mzuri wa elimu ya awali kutokana na shule
nyingi kuwepo mbali na makazi hivyo
kupelekea wazazi wengi kushindwa
kuwapeleka watoto wao katika shule za awali.
“ zipo sababu nyingi zilizo pelekea kuanzishwa kwa vituo
hivyo kama vile umabali wa kutoka makazi ya watu mpaka zilipo shule na kuwepo
kwa vijito vingi na milima ambayo kwa watoto wadogo hawawezi kwenda shule hizo”Alisema
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo EQUIP-TANZANIA mkoa wa
mara Kiangi Elifadhi alisema mradi huu umedhaminiwa na DFID-UKAID toka Uingereza na kuwa mradi huu upo katika
shule zote za msingi katika mikoa tisa
ambayo ilikuwa chini kiufaulu.
Alisema mradi huu ni wa miaka sita ambapo kwa awamu ya
kwanza walianza na mikoa ya Mara,Simiyu,Shinyanga,Tabora,Kigoma,Lindi na domama
na kwa awamu ya pili mradi huu utafanya kazi na mikoa ya Singida na Katavi.
Aliongeza kuwa miradi hii yote inagarimu kiasi cha shilingi
billion 184 ambapo kwa awamu ya kwanza uligarifu kiasi cha shilingi billion 136
na kwa mikoa milili iliyo ongezeka
itagarimu kiasi cha silingi billion 48 kwa mradi wa miaka miwili.
Elifadhi alisema kuwa wananchi wanajukumu la kuchangia
katika ujenzi wa madarasa katika vituo hivyo vya utayari na inapokuwa shule
shikizi basi mradi unaongezea nguvu kwa kutoa kiasi cha million 60 kwa
kuongezea nguvu za ujenzi kwa kila kituo.
Kwa upande wake mratibu wa mpango wa utayari kuanza
shule(SRP)Tabu Lazaro alisema kuwepo kwa vituo hivi 3 katika kijiji cha
mogabiri kata ya kitare kumewezesha kwa kiasi kikubwa kwa watoto wengi kuweza
kufika shule kwani vizuizi vilivyokuwepo awali vimepata ufumbuzi kwa watoto hao.
Aliongeza kuwa wazazi wamekuwa na mwamko wa kuwapeleka
watoto wao katika vituo hivyo vya utayari na kuhamasika pia katika ujenzi wa
vituo hivyo kwa kushindana katika mitaa yao kwani waliweza kugawana madarasa ya
kujenga kwa mitaa hivyo kuweza kuhamasishana wao wenyewe.