Mwanajeshi auawa na Polisi kwa Kupigwa Risasi Njombe

ASKARI wa jeshi la wananchi kikosi cha 514 KJ Makambako Mkoani Njombe ameuwawa kwa kupigwa Risasi na askali wa jeshi la polisi ambao walikuwa ni wachumba baada ya kutokea kwa ugomvi baina yao.

Askari wa jeshi la Polisi H 2299 Zakaria Dotto (25) amempiga risasi mbili askali wa jeshi la Wananchi Neema Masanja (25) Mkazi wa Mtaa wa Jeshini kata ya Maguvani mjini Makambako mkoani Njombe Njanda za juu kusini mwa Tanzania.


Inadaiwa walikuwa katika harakati za kufiukia hatua ya kuoana.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Kamishina Msaidizi wa Polisi Prudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa amekimbia baada ya mauaji hayo na kwa sasa anatafutwa na jeshi hilo kujibu tuhuma dhidi yake


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo