Hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani nchini Kenya Francis Andayi alisema mshtakiwa alimtendea unyama msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 aliyemvizia akitoka kununua bidhaa dukani.
Kiongozi wa mashtaka Bw Solomon Naulikha alimweleza hakimu kwamba mshtakiwa alikutana na mlalamishi kisha akamshika na kumpeleka katika jengo ambalo halikuwa limekamilika kujengwa na kumbaka kwa zamu akiwa na wavulana wengine.
“Lazima wenye tabia kama yako wajue kuna sheria inayowalinda wasichana na wanawake kwa jumla. Hupaswi kumtia kumbaka msichana au mwanamke,” alisema Bw Andayi.
Hakimu alitupilia mbali ushahidi wa mshtakiwa kwamba alikuwa na uhasama na jamii ya mlalamishi ndipo wakamwelekea.
“Ushahidi uliowasilishwa ulithibitisha wewe ulimbaka mlalamishi baada ya kumweleza umekuwa ukimtamani kwa muda mrefu,” alisema Bw Andayi.
Mshtakiwa aliamriwa awe akifanyakazi ngumu gerezani ndipo iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama yake.