NA
CHRISTINA MWAGALA, OMJ
Meya
wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa
mualiko wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili utakaofanyika katika mji wa Bashar.
Aidha
Meya atapata nafasi ya kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan
Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar
utakao husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.
Katika
mkutano huo ambao utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada
ya mkutano huo ataelekea mjini Teherani
kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo Muhammed Bakir Galbaf ambapo
pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara katika majiji hayo
mawili.
Aidha
katika mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo
kwenye majiji na namna ambavyo wanaweza kuyatatua.
“
Iran na Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba
mambo mengi wamekuwa wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji
haya mawili kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na
wananchi na wao wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.
Aliongeza
kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu
ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni
mmoja wapo.
“
Kushudia kwangu kampeni sio kwamba nataka kugombea nafasi ya urais hapa nchini ,
hapana ila ni moja ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao”
alifafanua.
Hata
hivyo Meya aliwasi wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni
kuchukua tahadhari kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na
mafuriko.