Mbunge wa Moshi Vijijini Kupitia CHADEMA Anthony Komu amesema hana mpango wa kukihama chama hicho na kujiunga na chama tawala (CCM)
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam Mbunge huyo amesema amekuwa akihusianishwa na kukihama chama hicho lakini yeye hajawahi kufikiria hivyo wala kuzungumza na CCM kuhusu kuhama chama hicho
Amesema hajawahi kushawishiwa kuhamia CCM na anachoamini hizo ni propaganda zinazoenezwa na CCM