Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gellasius Byakanwa ameshangazwa na tabia ya wanafunzi wa kike mkoani humo kutumia kinga za ujauzito,
Kufuatia vitendo hivyo Mkuu huyo wa mkoa amezitaka mamlaka husika kuzichukulia hatua maduka na zahanati zinazohusika kutoa huduma hiyo kwa watoto chini ya miaka 14.
Imeelezwa kuwa wanafunzi hao hutumia kinga hizo kama njia mojawapo ya kuzuia wasipate mimba ili hali sheria za nchi zinakataza watoto kushiriki vitendo vya ngono kabla ya umri wao