kutoka kwa jirani zetu Uganda kwa President Museveni ni issue ya Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50, ambaye ni muuzaji wa vyakula amethibitisha kwamba utajiri sio sababu ili uweze kuoa wanawake wengi.
Mohammed Ssemada anayetoka katika kabila la Wagisu nchini Uganda amefunga ndoa na wanawake wa tatu, Salmat Naluwugge, mwenye umri wa miaka 48 ambaye ana watoto wa 5, dada yake Naluwugge ,Mastulah Nawanje 24, pamoja na Jameo Nakayiza 27.
Harusi hiyo ilifanyika katika mji Wakiso huku umati wa watu walioshuhudia wakibaki mdomo wazi.
Kilichowashangaza wengi ni kwamba mke wa kwanza Naliwugge ni mama wa watoto 5 na amekuwa katika ndoa na Ssemada kwa muda wa miaka 20.
Ingawa Ssemada amethibitisha kwamba yeye kipato chake ni cha chini ila alionesha furaha kubwa kwa wake hao waliomkubali licha ya kipato chake hicho duni.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, Naluwugge alimshukuru Mungu kwa kuifanikisha harusi hiyo, ”Namshukuru mume wetu kwa kutuoa soote kwa siku 1. Kwangu, ni ishara tosha kwamba hatambagua yeyote”.