Licha ya Jeshi la polisi mkoa wa kusini Unguja kupambana na ajali za barabarani bado madereva wanaendelea kupoteza maisha ya watu na kuwaachia majeraha kufuatia ajali ya Gari Aina ya haise kugongana na Gari ya jeshi la wananchi wa Tanzania huko kidimni wilaya Ya kati mkoa wa Kusini unguja .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja Makarani Khamis Ahmed amesema kuwa ajali hiyo iliyotokea asubuhii ya Leo iliyohusisha Gari ya abiria aina ya haise yenye Namba za usajili Z. 675 roti namba 227 Machui imeigonga gari Ya jeshi la wananchi Tanzania yenye Namba 5937 JW12.
Ameongeza kusema chanzo cha ajali hiyo kuwa dereva wa Gari ya abiria ameshindwa kuchukua tahadhari za msingi kabla Ya kuingia kwenye barabara kuu na ndipo alipotoka na kuigonga gari ya jeshi la wananchi wa Tanzania .
Hata hivyo Kamanda makarani amesema kuwa upande wa majeruhi hadi sasa mmoja wao Kati ya sita hali yake ni mbaya na yupo hospitali katika chumba cha ICU na wengine amewataja majeruhi hao kuwa saidi Ali ,Abdallah said, Fatma Ali ,mtoto Iptisam wa miezi mitatu ambae amejeruhiwa kidogo.
Kamanda Makarani ametoa wito kwa madereva wa magari Ya abiria pamoja na magari mengine wanapoingia kwenye barabara wachukue tahadhari na kuwa makini pamoja na kuheshimu sheria na kanuni za barabara ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Rauhiya Mussa Shaaban.