Waziri Mkuu ahani Msiba wa katibu mkuu wa CWT

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma Jijini Dar es Salaam. 
Bw. Msulwa  amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.
Waziri Mkuu amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.
“Wote tumeguswa na msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.”
PMO_7858
Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .aliye simama kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa  pamoja na Mke wake  leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma Jijini Dar es salaam
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
PMO_7864
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuangalia Mke wake Mama Mary Majaliwa  wakati akisaini kitabu cha maombolezo,walipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma jijini Dar es salaam.
PMO_7870
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Sharifa Msulwa. kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa  ,Waziri Mkuu alifika nyumbani kwa Marehmu Toangoma  jijini Dar es salam leo November 18, 2017


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo