Wawahi kupiga kura ili waendelee na shughuli nyingine


Watu wamejitokeza kwa wingi katika upigaji kura wa udiwani Kata ya Bomambuzi mjini Moshi.

Mwananchi imefika katika baadhi ya vituo vya kupigia kura majira ya saa moja asubuhi leo Jumapili na kushuhudia wananchi wakiwa katika mistari kwaajili ya kupiga kura.

Baadhi ya wananchi wamesema kuwa wamelazimika kuamka asubuhi na mapema kwenda kupiga kura ili waendelee na majukumu mengine ya kimaendeleo.

Bakari Hamisi amesema kuwa yeye amehamasika kuwahi kupiga kura kwa sababu ni haki yake ya msingi na aendelee na kazi zingine za kila siku.

Hamisi amesema kuwa hali ya utulivu imetawala katika kituo alichopigia kura.

Ulinzi umeimarishwa katika vituo vyote vya kupigia kura licha ya kuwapo kwa mikwaruzano ya kiubinadamu kati ya wananchi na askari katika vituo hivyo.

Hadi sasa wananchi wanaendelea kujitokeza kupiga kura kwa wingi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo