SIDO kusaidia wajasiriamali

Image result for sido logoKatika kukabiliana na changamoto za ajira nchini Shirika la viwanda vidogo vidogo nchini (sido) mkoani Mara limeazimia kuendeleza viwanda vidogo vidogo hasa maeneo ya vijijini.

Hayo yamebainishwa na meneja wa sido mkoani hapa Winifrida Mungulu wakati akiongea na blog hii jana alisema wao kama shirika kazi yao kubwa ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuanzisha viwanda

Alisema sido inasimamia viwanda vyote venye mtaji wa kuanzia million 5 hadi mtaji wa million 200 na mtaji unapokuwa umevuka kiasi hicho basi kiwanda hicho kinakuwa hakipo chini yao tena.

Aliongeza kwa kusema kazi nyingine zinazo fanywa na sido ni kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo kwa kuwakusanya katika vikundi vyao na kuwapa elimu za ujasiliamali kwa wao kuchangia garama kidogo kwa ajili ya mafunzo hayo.

Mungulu alisema kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 wametoa mafunzo kwa watu 457  ambao wamepata mafunzo ya uselemala,ujasiliamali,utengenezaji wa sabuni na batiki pamoja na usindikaji wa vyakula .

Kati ya hao wapo ambao wameanzisha viwanda vyao na wao kama sido wapo nao bega kwa bega kwa ajili ya kuhakikisha wanapata nembo ya ubora wa bidhaa zao(TBS).

Aliongeza kuanzia 2015 -2017 tayari viwanda vidogo vipatavyo 22 vimeanzishwa katika mkoa wa mara kati ya vivyo viwanda  vingi ni vya usindikaji  chakula na nafaka .

Mungulu alisema kuwa mbali na viwanda hivyo bado wameweza kuwawezesha wanawake wa butiama katika kijiji cha kiabakari ambao wapo katika mfumo wa kongano kuwapatia vyerehani kwa ajili ya kufanyia kazi zao.

Alisema kuwa mradi huo wa kongano unafadhiliwa pia na shirika la TFSR CYMRU kutoka marekani wao wanagawa vyerehani kwa wanawake ambao wapopamoja na kwa kuanza mradi huo wameanzia kiabakari kwa kutoa cherehani 40 kwa kila mwanachama kuchangia shilingi elfu 50 na shirika kumalizia kiasi kinachobakia.

Mungulu alisema kuwa tangu july 2016 hadi sasa wametoa mkopo wa kiasi cha shilingi  million 194,750 kwa wajasiliamali 91 ambao wameomba mkopo na kupatiwa kutoka sido  na wao kama sido riba yao ya mkopo ni asilimia 18 ya mkopo wote unaokuwa nao.

Aliongeza katika swala zima la mkopo zipo changamoto nyingi zinazo wakabili kwakuwa wakopaji wengine huwa hawazingatii muda wa maerejesho yao,pamoja na hilo kuna changamoto ya elimu ya matumizi ya fedha za mkopokwa wakopaji wengi.

Na Asha Shaban


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo