Askari wawili wa Jeshi la Polisi wanaofanya kazi za doria za Utalii kisiwani Zanzibar wameondolewa katika kitengo hicho cha doria kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mahmoud amechukua hatua baada ya uwepo wa malalamiko kwa baadhi ya wananchi kuhusiana na tabia za rushwa.
Askari hao wamelalamikiwa kuomba na kuchukua rushwa kutoka kwa watalii katika Ukanda wa fukwe za Nungwi na kusababisha kero kwa wawekezaji wa maeneo hayo.
Wakati agizo hilo likitakiwa kuchukuliwa hatua mara moja pia Mkuu huyo ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa askari hao
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi