Tumemsoma sana kwenye vichwa vya habari kuanzia wiki iliyopita baada ya kwenda kwenye mnada wa nyumba za mabilioni na kushinda nafasi ya kununua nyumba 2 za zaidi ya Bilioni 2 lakini baadae akakamatwa na Polisi kwa kutokua na pesa mfukoni.
Jioni ya leo November 14 2017 Polisi Dar es salaam imemuachia kwa dhamana Dr. Shika baada ya kumshikilia toka wiki iliyopita kwenye kituo cha Polisi kati siku kadhaa tu baada ya kusema atashughulikiwa kama Muhalifu mwingine na kufikishwa Mahakamani.
Inawezekana ukajiuliza imekuaje mpaka ameachiwa? Kamanda Mambosasa wa Kanda Maalum ya Dar es salaam amesema “Amepata dhamana…. amejidhamini mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kumdhamini, dhamana yake ilikua wazi”“
“Baada ya dhamana anatakiwa kuripoti Polisi kila siku na hata kesho utaratibu kutoka kwa Mwanasheria ukikamilika tutampeleka Mahakamani” – Kamanda Mambosasa