Usiku wa kuamkia leo Nyalandu ametumia ukurasa wake wa twittter ambao ameonyesha hofu yake na kudai kwamba njia zote zinatumika kuhakikisha ananyamazishwa.
"Napokea idadi isiyo ya kawaida ya vitisho tangu kuondoka CCM chama cha tawala. Ni ajabu kuwa kuna hofu kubwa kutoka kwa wasomi, ambao wanatumia njia zote zinazowezekana kuninyamazisha" Nyalandu
Ameongeza "Tafadhali niombeeni mimi pamoja na familia yangu wakati wa majaribu haya tunayopitia".
Kabla ya kuhamia Chadema mapema mwanzoni mwa mwaka huu, Nyalandu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM.