Update
>>>Mlituaminisha kuwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kupitia TBC ni gharama kubwa na pia wananchi wanatakiwa kujikita kufanya kazi na sii kufuatilia bunge. Lakini ikumbukwe pia taasisi ya Tanzania Media Foundation (TMF) ilijitokeza kulipia gharama hizo. Je mko tayari kuwaruhusu TMF walipie gharama za kuonyesha bunge mubashara(Live)?
Mwakyembe anasema Swala la Live coverage lipo na Bunge ninaonyeshwa na ikitokea mambo muhimu linaonyeshwa. Ila hii ni serikali Mpya na imekuja na sera mpya. Watanzanania wanashangaa Bunge alionyeshwi live hawashangai sisi hatusafiri na hata kwenye vikao hakuna posho
Na akipatiakana mtu ambaye anaweza kurusha live aje kuongea nasi kwamba tuna pesa hii tuone kama wataweza kumudu live coverage hata kwa wiki moja. Waje tuongee nao waache porojo tu na kujigamba.
>>>Toka umekuwa waziri, umefanya jitihada gani kuboresha kituo hiki cha TBC na umejipangaje kufanyia kazi changamoto za Picha zisizo na muonekano mzuri (Angavu) na habari zinazobagua kwa lengo la kuipendelea serikali?.
Mwakyembe: TBC ndio shirika pekee ya utangazaji ambalo lina cover eneo kubwa sana Tanzania. Na tumebakiza robo ya nchi kuweka minara. Vinaja wanafanya kazi kubwa sana kuboresha vipindi vyao.
Mwaka huu wa pesa tumeweka pesa kuongeza usikivu wa TBC, Meneo ya Nyasa, Lushoto, Namanga na hata Kakonko
>>>Gabriel Zacharia wa TBC alipotangaza fake news juu ya Rais wa nchi aliadhibiwa yeye pamoja na wafanyakazi wengine na sio TBC kufungiwa, mbona magazeti yanafungiwa wakati kosa ni la mwandishi mmoja kama ilivyokua kwa Gabriel Zacharia?
Mwakyembe: Hakuna gazeti ambalo limefungiwa bila kuonywa kwa zaidi ya mara sita. sasa naomba tuambie kituo cha TV ambacho kumepotosha halafu tukakionyoa kama mara 5 au 6 natukakiacha
>>>Kwanini Kifungu 59 kimetumika kufungia gazeti wakati kinampa uwezo wa kufungia maudhui tu?
Mwakyembe: Unajua mimi na Msemaji wa Serikali tuna nyazifa tofauti. sasa naomba siku tupate muda na sisi tuje na ushahidi wetu, pengine vyombo vya habari vilivyofanya makosa tuvihoji mbele ya watu. Maana watu wanaweka habari bila source
>>
Niliwambia waandishi wa habari wajaribu kuwasiliana na Wizara yake. Ukiwa na shida nenda wizarani jenga hojan Wizara yangu ipo wazi masaa 24. Njoo tuzungumze tujenge hoja
>>> Kupitia sera sheria za ulaya zimejenga ajira nyingi kwa Ulaya. Serikali imejipanga vipi kuhusu hilo?
Mwakyembe: Kwenye michezo ni sehemu ambayo tukijipanga watanzania wanaweza kupata ajira sana. Kupitia waziri mkuu tunataka kuanzisha michezo na kutoa kipaumbele kwenye michezo ya sekondari na primary na itaenda bila kusimama ili kulea vipaji.
Sisi ni wenyeji wa AFCON 2019 kwa vijana Watanzania watashangaa ni wazuri kuliko vijanalipita. Na viwanja vile tutavibadili nyasi maana zimeshachoka.
Sasa hivi tunaweka misingi kuhakikisha tunaonekana Duniani.
>>Kukataliwaa Zanzibar CAF na FIFA kunarudisha nyuma maendeleo katika soka, unawasaidiaje?
Mwakyembe: Tumepigana sana kuhakikisha kuwa Zanzibar inakuwa mwanachama wa CAF na FIFA ila wao wamekataa. Hivyo tumechukua hatua kadhaa tumetuma ujumbe na tusingependa hili swala kuzungumziwa sana maana wenzetu wao wana uwezo mkubwa sana. Ila tunalifanyia kazi
>>>Je sheria inaweza kuwalinda vipi wanafunzi juu ya swala la hati miliki?
Mwakyembe: Kama umefanya utafiti fulani ukiwa chuoni au shuleni basi huo utafiti ni mali ya hiko chuo. Na kama unafanya kazi sehemu fulani ukagundua basi wewe na muajiri wako mnahusika
Mambo ya stika kwa wasanii, mimi niliwakusanya wasanii na kuwaambia tuhamie kwenye swala la Tehama. Kama kuna mtu analeta shida kuhusu stika aje wizarani au aende Basata
>>>Vazi la Taifa lilishia wapi?
Mwakyembe: Serikali ilikuwa inaogopa kuwapangia watanzania kuhusu vazi la taifa, na tuliacha watanzania waibue wenyewe vazi la taifa. ila kama watanzania wanahitaji vazi la taifa basi kupitia wawakilishi wao walibue tena na kujadili
>>>Kuhusu wanamuziki kuimba nyimbo za siasa, je wanaruhusiwa iwe kukosoa au la?
Mwakyembe: Ukitaka kufanikiwa katika sanaa hebu usijiingize wewe kujifanya ni mwana siasa. imba nyimbo za kawaida ambazo haziusiani na siasa. ukitaka kuwaiga wana siasa wanaweza kukuponza maana wewe ni mwananchi wa kawaida na wabunge wana katiba inawalinda.
Ila imba unachotaka na wala usitukane watu, ukiimba ujinga sio lazima serikali hata wananchi watakukosoa.
TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU NA ASANTENI KWA KUWA NASI. TUKUTANE TENA IJUMAA IJAYO KWA KIPINDI HIKI TUNAPOKUWA NA WAZIRI TOKA WIZARA NYINGINE
