Jeshi polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu kumi na moja akiwemo mmiliki wa taasisi ya elimu ya
Scolastika kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha pili Humprey Makundi ambaye
amebainika kufariki
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro ACP Hamisi Issa amesema kwa sasa wamepata kibali cha mahakama cha kufukuwa
mwili wa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 ambao umezikwa katika makaburi ya manispaa ya Moshi na
kuhifadhiwa Mochuari kwa ajili ya uchunguzi.
Amesema mpaka sasa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo pamoja na watuhumiwa
wanaosadikiwa kuhusika katika kifo chake ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Aidha kamanda Issa ametoa onyo kali kwa wamiliki wa shule ambao wamepewa dhamana ya kulea watoto.
Mzazi wa mtoto huyo Bw.Jackson Makundi amesema amesikitishwa na taarifa za kupotea kwa mtoto wake ambapo
ameomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika
kuhusika na kifo hicho.