AUDIO: Agizo la Mkuu wa Mkoa laibua Mjadala Baraza la Madiwani Makete

Serikali imesema haijapuuza maagizo ya kuwapeleka watumishi katika kituo cha upasuaji cha Lupila wilayani Makete mkoani Njombe

Akitoa majibu ya hoja katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete ya kukosekana kwa watumishi katika kituo cha upasuaji katika kituo cha afya Lupila, Kaimu Mkurugenzi mtendaji Bw. Gregory Emmanuel amesema tayari mtumishi mmoja ameshapelekwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya kazi

Amesema kutokana na agizo la Rais John Magufuli la kutomhamisha mtumishi pasipo kumpa fedha za uhamisho, wanalazimika kuwapeleka watumishi hao kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo pia wiki hii wanatarajia kumpeleka mtumishi mwingine

Miezi michache iliyopita Mkuu wa mkoa wa Njombe Christophel Olesendeka alifungua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Lupila na kuagiza watumishi wapelekwe mara moja katika kituo hicho

Sikiliza sauti hii hapa chini>>>>>


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo