Mchungaji atumia pombe kubatiza waumini

Mchungaji mmoja huko Afrika Kusini amekuwa akikosolewa vikali baada ya kuanza kubatiza washirika kwa kutumia vilevi ambavyo wanavipenda kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu

Askofu Tsietsi Makiti, (52) ambaye pia  ni Mwanzilishi wa kanisa hilo linalojulikana kama 'Gabola', amesema kuwa ameongozwa na maandiko katika Biblia ambapo Yesu alibadilisha maji kuwa divai.
"Watu wanao kunywa na kubatizwa na bia wana furaha na amani. Hii inamaanisha kuwa wanaishi katika kivuli cha Mungu, "alisema Makiti.
Kanisa hilo lenye jina 'Gabola' jina likimaanisha 'Kunywa' limesema linakubali kuwapokea waumini waliotoka makanisa mengine huku likiweka wazi kwamba idadi ya watu wameongezeka kufikia 500 ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.
Waumini pia wanaruhusiwa kunywa wakati huduma za kanisa zikiendelea.
Aidha Askofu huyo ameweka wazi kwamba ana mipango ya kuanzisha matawi ya kanisa lake hilo katika miji mbali mbali


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo