Wananchi kumuweka askari chini ya ulinzi

Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Bw. Nico Mwakasanga ameamuru kukamatwa kwa askari polisi aliyejulikana kwa jina la Bw. Mbunda na kuwekwa ndani kwa uchunguzi baada ya baadhi ya wananchi kutoa malalamiko kwa mkuu wa mkoa Mh.Christina Mndeme kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji na askari huyo. 

Wakitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Christina Mndeme ambaye kwa mara ya kwanza amefanya ziara ya kikazi wilayani Tunduru tangu kuteuliwa kwake Octoba  kushika wadhifa huo, baadhi ya wananchi hao wa Tunduru wamesema askari huyo amekuwa akiwanyanyasa kwa kuwabambikiza kesi na wakati mwingine kukamata wananchi wakiwa kwenye shughuli za uzalishaji mali akiwaita wazururaji.
Akijibu malalamiko hayo ya wananchi, Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi, Mwakasanda amesema ameshaagiza askari Polisi huyo akamatwe popote alipo na kuwekwa ndani kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh, Christina Mndeme amewaonya askari polisi kuacha tabia ya kubambikizia kesi wananchi na badala yake watende haki huku akiwataka wananchi wasiogope kutoa taarifa polisi endapo wanafanyiwa vitendo hivyo ili hatua zaidi zichukuliwe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo