Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba Haji Manara amesema anashangazwa na watanzania wanaoibeza Simba pale inapokuwa haijashinda mechi inazocheza
Amesema hata timu ya Simba ingewasajili Ronaldo na Mesi na Kocha akawa Sir Alex Furgerson na Kocha msaidizi akawa Jose Morinyo bado timu hiyo haitashinda kila mechi
"Mi nimekuwa nikishambuliwa sana, hasa Simba inapotoa Sare, jamani mi najiuliza hivi watanzania wanajua mpira kweli, sasa sijui ndio nawatukana lakini najiuliza hivi wanajua mpira kweli? hawa watanzania ni watu wa wapi? amesema Manara
Amesema kwa sasa wanapitiia taarifa ya Kocha wao Omog kuangalia mapendekezo yake ili waweze kufanya usajili kama itahitajika kufanya hivyo kwa mapendekezo ya kocha huyo