Majimbo na Kata zilizoko wazi kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo tena

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kufuatia, Lazaro Samwel Nyalandu kujivua Uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge.

Aidha, kwa mujibu kifungu cha 113(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume imepokea Hati ya Mahakama Kuu ya Tanzania ikithibitisha uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge wa Jimbo la Longido ambalo, Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mbunge.
 
Wakati huo huo Waziri wa Tamisemi kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata tano zilizopo katika Halmashauri mbalimbali.
 
Hata hivyo, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatoa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi wazi za Majimbo na Kata hizo hapo baadae.
 
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo
Majimbo na Kata zilizo wazi ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyowazi
NA.MKOAHALMASHAURIJIMBO
1.SingidaHalmashauri ya Wilaya ya SingidaSingida Kaskazini
2.ArushaHalmashauri ya Wilaya ya LongidoLongido
Jedwali Na. 2: Kata zilizowazi
NA.MKOANA.HALMASHAURINA.KATA
1.Kagera1.Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.1Keza
2.Arusha2Halmashauri ya Jiji la Arusha2Kimandolu
3.Pwani3.Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.3Kurui
4.Tabora4.Halmashauri ya Wilaya ya Tabora4Bukumbi
5.Tanga5.Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.5Kwagunda

Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
 TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
16 NOVEMBA, 2017


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo