MADEREVA WA BODABODA MKOANI IRINGA WAPATIWA ELIMU NA PIKIPIKI BURE KUDUMISHA DORIA


 Cheti cha uhitimu wa mafunzo wa udereva wa Pikipiki.
WAHITIMU wa mafunzo ya udereva mkoani Iringa, wamepatiwa Pikipiki za bure kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi usalama barabarani na kwa kundi hilo ambalo limekuwa likilalamikiwa kutofuata sheria za usalama wa barabara na hivyo kusababisha ongezeko la ajari.

Akikabidhi msaada wa Pikipiki mbili katika ukumbi wa Hallfear kwa uongozi wa chama cha waendesha Bodaboda mjini Iringa, mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama mkoani Iringa Bw. Salim Abri “Asas” amesema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi yake kwa chama hicho cha waendesha Bodaboda, pekipiki ambazo zitatumika katika dolia.

Bw. Salim amesema msaada huo ni katika kutambua umuhimu  kazi hiyo ya udereva wa Pikipiki ambao kwa kiwango kikubwa umetoa ajira kwa kundi kubwa la vijana nchini.

Salim amesema kamati yake ya ulinzi na usalama barabara itahakikisha ajira hiyo inakuwa salama kwa kutoa elimu kwa madereva wa pikipiki kwa lengo la kupunguza ajali na vifo vitokanavyo na usafiri huo.

Aidha wahitimu hao 100 wa mafunzo ya udereva wamelipiwa ada ya elimu hiyo ya udereva huku mwenyekiti huyo akitoa nafasi nyingine kwa madereva 100 ambapo pia wartapatiwa elimu hiyo.

Hata hivyo Bw. Salimu ameahidi kuongeza msaada wa Pikipiki nyingine mbili ili kuifanya kazi hiyo ya dolia kwa uhakika na kufanikisha mpango wa kutokomeza ajali na vifo vitokanavyo na usafiri huo wa pikipiki., huku akiwataka madereva hao kutobweteka kwa kuishia kazi hiyo ya udereva wa Pikipiki bali kufanya jitihada za kusonga mbele.

“Sidhani kama kazi hii ya udereva wa Pikipiki mtafanya hata muwapo wazee, cha msingi mnachopaswa kukifanya ni kuwa na mawazo ya kusonga mbele muwe madereva wa magari, msiishie hapa kwenye kazi hii ya bodaboda tu!! Lakini ipo haja ya kuanzisha Saccos yenu ili muweze kukopeshana fedha na kuweza kumiliki Pikipiki zenu, maana ninaambiwa kuwa hapa baadhi yenu Pikipiki hizi siyo zenu,” Alisema Salim.


Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani kupitia jeshi la Polisi (OCD)  SP Panfil Honono amewataka madereva hao kuwa na nidhamu katika kazi hiyo na kusimamia sheria za barabarani bila shuruti ili ajira hiyo iwe na thamani katika jamii.

Naye mwakirishi wa Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Iringa SP Zakaria Benard amewataka madereva hao kujihami katika kazi hiyo, kwa kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa ikiwa pamoja na kuacha tamaa ya kuwachukua abiria wanaowatilia shaka.

“Mtu kama humfahamu siyo lazima umpeleke anakotaka, lakini pia muwe makini kwa kuwatambua wateja wenu, muulize jina huku ukimuhoji baadhi ya maswali, ambavyo yatakuwa ni msaada kwako, kitu kingine ndugu zangu!! Acheni tamaa, mfano unakuta mteja humfahamu anakukodi umpeleke kituo kimoja, unafikanae katika kituo kile alichosema nataka kufika, anasema umpeleke mbele zaidi, hapo utambue kuwa huyo siyo abiria mwema, kataa na kisha muache hapo na urudi katika kituo chako, tunafahamu kumekuwa na wimbi la utekaji na hata mauaji mnafanyiwa kwa kutumia njia hizo za kuwakodi ili wawapole pikipiki, kwa hiyo hapo kuweni makini na waangalifu sana,” alisema SP Zakaria.
 
Na Oliver Motto, Iringa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo