Dayosisi ya Kusini Kati Yapata Askofu Mpya

Dayosisi ya kusini kata imefanya uchaguzi wa askofu kwa  mujibu wa katiba ya kanisa na Mchungaji Wilson sanga amechakuwa kuwa askofu wa dayosisi hiyo

Akizungumza baada ya uchaguzi huo uliofanyiaka hapo jana katika makao makuu ya dayosisi hiyo Msaidizi wa askofu Mchungaji Adili Pagalo ambaye amechaguliwa tena kuwa msaidizi wa askofu amesema ndugu Wilison Sanga amechaguliwa kuwa askofu wa Dayosisi ya kusini kati ambaye amewahi kuhudumu kama katibu mkuu wa Dayosisi hiyo  ambapo watu watatu waliwania kiti hicho katika uchaguzi huo  pia umefanyika uchaguzi  wa wakuu wa majimbo 
Awali Dayosisi hiyo ilikuwa ikiongozwa na  Askofu Levisi Sanga ambaye ameiongoza dayosisi hiyo kwa mika minne na msaidizi wake akiwa Adili Pagalo ambaye amechaguliwa tena
katika mkutano huo pia umehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwepo  Mkuu wa kanisa la kiinjili la Kilutheli tanzania KKKT askofu Fredrick Shoo ambaye pia ni askofu mkuu wa Dayosisi ya kaskazini na msemaji mkuu wa neno Askofu Dk Alex Malasusa ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya mashariki na Pwani
kwa mujibu wa katiba ya kanisa hilo askofu aliye chaguliwa atahudumu kwa miaka kumi huku wakuu wa majimbo wakihudumu kwa miaka minne pekee


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo