Mpya: Wachina Wanne Mbaroni na Makinikia

Jeshi la polisi mkoani Mara limefanikiwa kukamata magari mawili aina ya NISSAN PICK UP yaliyobeba masanduku 14 ya mchanga wa madini (MAKINIKIA) wakiwamo raia wanne wa kichina ambao ni wawekezaji wa mgodi wa zem Tanzania Co. L.T.D uliopo Nyasirori wilayani Butiama wakiwa katika harakati za kutorosha mchanga huo wenye uzito wa kilo 700
Akithibitisha kutokea kwa tukio kamanda wa jeshi la polis mkoani Mara ACP JAFARY MOHAMMED amesema ilikuwa ni majira ya saa 11 alfajir askari wake walipofanikiwa kuwakamata raia hao wa kutoka china wakiwa na magari mawili aina ya Nissan pick up yaliyobeba shehena hiyo yenye uzito wa kilo 700 baada ya kuweka mtego katika eneo la kiabakari.
Kufuatia jaribio la utoroshaji wa makinia hayo kamanda wa jeshi la polis acp jafary mohammed akatoa wito kwa wamiliki wa migodi kutothubutu kujihusisha na usafirishaji wa madini au mchanga wa madini kinyume cha sheria.
Tukio la kukamatwa kwa mchanga wa dhahabu (Makinikia) ni mwendelezo wa kazi kubwa ya inayofanywa na rais john pombe magufuli katika jitihada zake za kuhakikisha rasilimali ya taifa inalindwa ipasavyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo