Wameagizwa wasitangaze tukishinda - Mashinji

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda.

Dkt. Vincent Mashinji amesema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya. 
"Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda" alisema Katibu Mkuu wa CHADEMA 
Mbali hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka.
"JPM kusema wapo watu waliokuwa ni wezi katika CCM na kusema saizi watu hao wamekimbilia CHADEMA. Lazima JPM ajue kuwa “Wameamua kuokoka” Alisema Mashinji. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo