Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Arusha kimetangaza kujitoa kwenye uchaguzi wa madiwani unaoendelea nchini hii leo kwenye kata 43, wakisema uchaguzi huo umekuwa wa hatari kwao
Akiongelea hilo Afisa habari wa CHADEMA Bwana Tumaini Makene, amesema wameona ni bora wajitoe kwenye uchaguzi huo ambao umedaiwa kugubikwa na vitendo vya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, ambazo zimelenga kukiharibia chama chao.
Makene ameendelea kwa kusema kwamba wakati uchaguzi ukiendelea mawakala wao walitolewa nje ya vyumba vya kupigia kura na kisha kurudishwa baada ya masaa manne kupita, kitendo ambacho wanakitilia mashaka.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi