Akamatwa kwa rushwa uchaguzi mdogo

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema jeshi la polisi limejipanga vizuri na limeimarisha ulinzi katika vituo vyote 24 vya kupigia kura kwenye uchaguzi wa udiwani kata ya Chipogoro wilayani Mpwapwa

Akizungumza kamanda Muroto amesema askari wapo wa kutosha katika vituo vyote pamoja na yeye akiwa anazunguka maeneo yote ili kuhakikisha uchaguzi unaendelee kwa amani na utulivu na hadi sasa hakuna changamoto yeyote ya kiusalama.
Aidha kamanda ameeleza kuwa kuna mtu mmoja amekamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU ambapo amesema ripoti kamili ataitoa baada ya uchaguzi kukamilika. 
"Mimi nipo eneo la kata ya Chipogoro nazunguka katika vituo vyote ila kuna ripoti ya wenzanetu wa TAKUKURU wamemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za rushwa hivyo nikirudi ofisini baadae nitatoa ripoti kamili", amesema.
Kwa upande mwingine kamanda ametoa rai kwa wananchi kuwa watulivu wakati wa kupokea matokeo na kama kuna mtu ambaye hataridhika na matokeo yatakayotolewa zipo taratibu za kufuata na sio kufanya fujo.
Kwa upande wake, Msimamizi wa uchaguzi Mohamed Maje amesema hakuna changamoto zozote zilizopatikana na mpaka sasa nusu ya wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura wamejitokeza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo