Wagombea CHADEMA watakiwa kujitoa

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewataka wagombea wote wa udiwani katika kata tano Arumeru Mashariki wajitoe katika uchaguzi huo

Mbowe ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha huku akisema kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vurugu.
Sambamba na hayo Freeman Mbowe amewataka mawakala wao wa uchaguzi katika vitup vya kupigia kura waondoke vituoni.
Leo wananchi wa Tanzania Bara wanapiga kura kuchagua madiwani katika kata 43 hapa nchini, lakini mpaka sasa kumekuwa na taarifa mbali mbali za uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kukamatwa ka baadhi ya wagombea na mawakala.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo