AUDIO: Walichokifanya wananchi wa Luwumbu kwenye barabara yao

Wananchi wa kijiji cha Luwumbu kata ya Luwumbu wilayani Makete mkoani Njombe wameamua kuingia barabarani kufukia mashimo katika sehemu korofi za barabara hiyo baada ya kuona mkandrasi anasuasua

Wakizungumza kupitia kituo cha Green FM wananchi hao wamesema wameamua kufanya hivyo baada ya kuna ukarabati unachelewa licha ya kuanzia maandalizi na baadaye akaondoka bila wao kuelewa sababu


"Unajua mtangazaji tabu tunapata sisi, mvua zimeanza kunyesha haya magari ya abiria yanayokuja huku yatashindwa halafu tabu tutapata sisi" amesema mwananchi mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake

Akijibu malalamiko hayo ya wananchi Diwani wa kata hiyo Mh Enock Ngajilo amesema ni kweli mkandarasi hiyo amesimama kufanya kazi kutokana na mabadiliko ya serkali kubadilisha barabara hiyo kuwa chini na wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA Lakini mkandarasi hiyo ataanza kazi hivi karibuni

Sikiliza sauti zao kwa kubofya hapa chini:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo