HAKIMU Mkuu wa Mahakama iliyo katika wilaya ya Luweero, Uganda ameagiza mwanamume afungwe rumande kwa kujiita 'Yesu Kristo’
Mwanamume huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Juliet Hatanga, mnamo Novemba 9, kwa mashtaka ya kuwa mwanachama wa kundi haramu na shtaka lingine la kusimamia kundi haramu.
Wakati huo alisema jina lake ni Joshua 'Yesu Kristo’.
Ilibainika alikuwa ameacha kutumia jina hilo Agosti 2016, akavunja kundi lake baada ya kushtakiwa kwa makosa sawa na hayo.
Alikamatwa tena mapema wiki iliyopita katika wilaya ya Luweero akitumia jina hilo hilo huku akidai hatambui mamlaka yoyote duniani ikiwemo ya Rais wa Uganda.
Alishtakiwa pamoja na wafuasi wake watatu ambao pia walikataa kujitambulisha kwa majina yao rasmi na badala yake wakasema wanaitwa Femera Shanita, Zomunu Parusha na Nuseni Dawunini.