AJENTI wa M-Pesa aliuawa kinyama Jumatano jioni mjini Moyale.
Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Kaunti ya Marsabit Waciira Mathenge aliambia Taifa Leo kuwa polisi wanafanya uchunguzi.
Bw Mathenge alisema mhudumu huyo alikuwa na majeraha mabaya, na aliaga dunia akipokea matibabu hospitalini.
Ajenti huyo wa kike alipata majeraha mabaya ya kukatwa baada ya kushambuliwa na watu wanaoaminika kuwa majambazi.
Majirani na polisi walijaribu kumuokoa na kumkimbiza hospitalini lakini hakupona
