Warombo kuamua juu ya Ben Saanane

Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini, amemtahadharisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kwamba wananchi wa jimbo lake hawajasahau tukio la Msaidizi wa Mbowe aliyepotelea kusikojulikana kwani bado wana hasira inayofukuta na kwamba hautaisha pasipo kufanya maamuzi.

Mhe. Selasini amesema kwamba yeye kama Mbunge wa Rombo na Ben Saanane akiwa ni mpiga kura wake analitaka jeshi la polisi pamoja serikali waweze kutoa ripoti ya kijana huyo kama bado yupo hai au ameshafariki ili wafanye matanga vinginevyo wao wataamua wenyewe cha kufanya.
"Nataka nimwambie IGP  Sirro na watanzania wote kwa ujumla ipo siku warombo tutaitana kufanya maamuzi, nataka niwaambie warombo damu ya mwenzetu haiwezi kupotea Halafu sisi tukakendelea kukaa kimya kama wajinga, Lazima tufanye maamuzi sahihi. Vijana wa Rombo popote pale mlipo nataka kuwaambia mwaka huu hautaisha lazima tukutane tuamue juu ya mwenzetu".... Selasini amesema
Hata hivyo Mbunge huyo ameeleza kwamba familia ya Ben Saanane imekuwa na huzuni tangu kupotea kwa kijana wao ambapo mpaka sasa jeshi la polisi halijawahi kutoa ripoti tangu taarifa za kupotea kwake zilipotangazwa 
Hata hivyo amesema kwamba kadiri watanzania wanavyoendelea kuteseka ndivyo ambavyo wanaendelea kukomazwa hivyo hali hiyo siyo njema kwa afya ya nchi kwani itafika kipindi kwamba nchi italipuka.
Ben Saanane ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, tangu kuripotiwa kupotea kwake ni takribani mwaka sasa ambapo si familia, jeshi la polisi au Chama chake wanajua ni wapi alipopotelea huku chama chake kikiendelea kuliomba jeshi la polisi na serikali kufanya uchunguzi kuhakikisha anapatikana.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo