Waandishi watangaza kususia habari zinazolihusu Jeshi la Polisi

Waandishi wa habari mkoani Geita wametangaza kususia kuandika habari zinazolihusu jeshi la polisi kutokana na kukithiri vitendo vya unyanyasaji kwa waandishi wa habari wanapokuwa kazini.



Uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kumalizika kikao cha dharula cha waandishi wa habari ambao walikutana ili kujadiliana namna bora ya kukabiliana na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari mkoani Geita.

Tamko la kuondoa ushirikiano kwa jeshi la polisi limesomwa na mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe (pichani),ambaye amesema uamuzi huo utatenguliwa iwapo uongozi wa Jeshi la polisi mkoani humo utajitokeza kuomba radhi kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na polisi pamoja na kuwahakikishia usalama wao wawapo kazini.

Aidha uamuzi huo umeanza kutekelezwa baada ya tamko hilo huku ikielezwa kuwa mwandishi wa habari atakayekiuka makubaliano hayo atachukuliwa hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kufutwa uanachama wake ndani ya Klabu hiyo.


Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku mbili zimepita tangu waandishi wa habari wanne kushambuliwa na kuharibiwa vifaa vya kazi wakati wakichukua matukio ya vurugu zilizotokea kwenye shule ya sekondari Geita(Geseco) ambayo pia wanafunzi walikuwa wakitishia kuichoma moto iwapo wenzao watano waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi hawataachiliwa huru na kulejea shuleni hapo.


Waandishi waliokutana na masaibu hayo na vyombo vyao kwenye mabano ni Editor Edward(Mtanzania),Rehema Matowo(Mwananchi),Ester Sumira(Azam Tv) na Emmanuel Ibrahimu(Clouds tv).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo