Mfanyakazi Apigwa Risasi kwa Tuhuma za kuiba Mafuta ya Kampuni

Na Amili Kilagalila
Wananchi wa kijiji cha Mselesele kilichopo wilaya ya Ludewa mkoani njombe wameandamana hadi kwenye ofisi za kampuni ya YUSHING inayofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya Njombe Ludewa kufuatia kupigwa risasi kwa Mfanyakazi mwenzao anayefahamika kwa jina la Haji Athuman kwa madai ya kuiba mafuta.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema kuwa amepokea taarifa hizo majira ya saa mbili asubuhi kuwa askari huyo wa ulinzi anaeitumikia kampuni ya Yushing  inayojenga barabara ya
kutoka Lusitu hadi Mawengi amefanya tukio hilo la kupigwa risasi kijana huyo kwa kushinikizwa na bosi wake anayefahamika kwa jina moja la SAMYU

Ni Hali ya taharuki ambayo imewakumba wananchi hawa wa kijiji cha Mselesele baada ya mfanyakazi mwenzao anayefahamika kwa jina la Haji Athmani kupigwa Risasi na Askari wa ulinzi anayefahamika kwa jina la Visent Samson Nguro mwenye namba MG.364122 ambaye inasemekana aliamriwa na mkalimani aliyefahamika kwa jina moja la Samyu ambaye ni miongoni mwa wachina waliopo katika kampuni hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Samyu  ni Miongoni mwa wachina Tisa waliopewa barua ya kuondoka nchini muda mrefu kwa kubainika kuwa wameingia nchini Tanzania kwa njia zisizo sahihi kupitia wachina walioomba ridhaa ya kufanya kazi ya
ujenzi wa barabara ya Lusitu - Mawengi nchini hapa.

Aidha imeelezwa kuwa Samyu pamoja na Askari aliye husika na tukio la kumpiga risasi Haji wameondoka na mgonjwa huyo bila ya ruhusa wala kibali chochote kutoka serikalini na kuelekea hospitali ya mkoa wa Njombe na baadaye akaondoka na mgonjwa huyo kuelekea Jijini Dar es salaam katika hospitali ya Muhimbili baada ya kupewa rufaa kutoka hospitali ya Kibena ya mkoani Njombe.

Swali la wananchi wengi ni kuwa Samyu anatajwa kuhusika na kupigwa risasi Kwa kijana Haji , na ndie alieondoka na mgojwa huyo pamoja na askari waliohusika na tukio hilo kumpeleka hospitali je, usalama wa Kijana Haji uko wapi? lakini pia najiuliza mahusiano ya wafanyakazi na kampuni yakoje mpaka haya yote yanatokea  ?  swali langu limekosa majibu baada ya viongozi wa kampuni wote kushindwa kunipa majabu ya kuridhisha kwamadai ya kuwa
msemaji wa kampuni hiyo yupo sarini.

Wananchi wa kijiji cha Mselesele ambao pia ni wafanyakazi waliokuwa pamoja na kijana Haji wansema kuwa wasikitishwa na tukio hili la mfanyakazi mwenzao kupigwa risasi Huku wakieleza kuwa hawana tena imani ya kuendelea kufanya kazi na Kampuni hiyo kwani wamekuwa wakifanyiwa vitendo vyaunyanyasaji ikiwemo kuwahitaji kimapenzi baadhi ya wafanyakazi wa kike ambao wamefukuzwa baada ya kugoma kuingiliwa kimwili na wachina hao.


Bille Musa ni mshauri wa Mradi huo wa ujenzi wa barabara inayojengwa na Kampuni ya USHINE inayoshirikiana na kampuni zingine tatu amesema kuwa Samyu na wenzake sita walishapewa barua za kuondoka nchini laki ni bado hawajafanya hivyo huku akieleza kuwa suala hilo lilishafikishwa Katika ofisi za Tanroad mkoani njombe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo