Mwanahabari aliyekuwa akisakwa na Polisi tangu Jumamosi Ajipeleka Mwenyewe

CENTRAL PRESS CLUB (CPC) 

Ndugu zangu wanahabari, pole na majukumu ya ujenzi taifa. 

Baadhi yetu tulikuwa na taarifa kuhusu mwandishi mwenzetu Agusta Njoji kwamba alitakiwa na wenzetu jeshi la polisi mkoani Dodoma tangu siku ya jumamosi kwa ajili ya kutoa maelezo ya kile walichokitaka.

Leo majira ya asubuhi polisi walifika Ofisi za IPP Media ambapo Njoji anafanya kazi na kwa bahati mbaya walikuta amekwenda katika majukumu mengine. Baadae mwandishi huyo alikwenda mwenyewe polisi akiongozana na mwandishi Sharon Sauwa.

Polisi walimhoji kwa taklibani saa 2 kabla ya kumweka nje kwa taklibani saa 3 zingine. Baada ya hapo walimtaka kuwa na mdhamini kama siyo basi awekwe ndani.
Mimi na waandishi wengine akiwemo Katibu wetu Bilson Vedastus tulifika hapo kwa nyakati tofauti kabla ya uamuzi wa kumweka ndani.

Namshukuru Mungu nilisimama kwa niaba yenu kumwekea dhamana kwa bondi ya 5 Mil, na sasa yuko nje hadi tar 25/10 siku ya jumatano saa 3 asubuhi.

MSINGI WA HOJA
Polisi wamemtaka walimtaka AGUSTA kueleza kuhusu habari ya magari ya washawasha aliipata wapi na hata alipowaambia kutoka PAC bado walimtaka awaeleze wabunge walioibua jambo hilo.

Bila kuingilia Uhuru wa chombo hicho muhimu kwa usalama wetu, lakini kitendo kilichofanywa si cha kiungwana kabisa.

Mosi: Toka jumamosi Njoji anatafutwa kama mwizi na mnyang'anyi
Pili: Wenzetu polisi wameshindwa kutafsiri kanuni za bunge kwamba kwamba walipaswa kumuuliza kwanza Mwenyekiti wa kamati ya bunge za hesabu za serikali (PAC) kama hilo lilitokea ndani ya kamati.

Pamoja na mambo mengine ambayo tutakuja kuyatolea ufafanuzi baada ya kunabaini kiini cha tatizo, CPC inalaani kwa nguvu zote kitendo cha polisi kitumia nafasi zao kutaka kuwapangia waandishi cha kuandika. Ikumbukwe kufanya hivyo ni kuingilia Uhuru wa mwanahabari na kubaka taaluma za wengine.

Jambo hili halikubariki, halitakubarika wala kuvumiliwa katika nafasi hizi ambazo sote tunategemeana katika majukumu.
Nimuombe Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kukutana na waandishi na kutupa ufafanuzi huu wa sintofahamu vinginevyo Waandishi hawatakuwa tayari katika ushirikiano uliodumu na chombo hicho.

Aidha, naiomba idara ya habari za bunge kutupa ufafanuzi ni wakati gani wa waandishi kuandika habari za bunge au kamati za bunge ili kuondoa sintofahamu hiyo itolewe tafsiri sahihi ya kanuni katika kuripoti habari za bunge.

Nichukue nafasi hii kuipongeza kamati ya PAC na mwenyekiti wake Naghenjwa Kaboyoka ambao wamekuwa nasi katika jambo hili kwa kila hatua.

Mwisho, nampa pole Agusta Njoji na kumtaka asife moyo badala yake apambane ili mradi asivunje miiko ya uandishi.

Habel Chidawali
Mwenyekiti CPC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo