Shehena hiyo ilikamatwa katika eneo la Namanga wilayani Longigo mkoani Arusha ikiingizwa nchini kwa njia za panya hatua ambayo watendaji wa kituo cha Namanga na wa idara ya mifugo mkoa wa Arusha wamesema hatua zaidi za kudhibiti vitendo hivyo zitaendelea kuchukuliwa.
Afisa Mfawidhi Mkaguzi wa mifugo Bw Medard Tarimo amesema vifaranga hivyo havikupaswa kuingizwa nchini na kwamba pamoja na kuteketezwa kwa vifaranga hivyo pia hatua zaidi zitaendelea kwa waliowezesha kufanikisha zoezi hilo na pia kwa gari lililotumika.
Kwa upande wake mtuhumiwa aliyekutwa na vifaranga hivyo vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya milioni 12 amesema amevinunua nchini kenye japo hakuwa tayari kueleza alikokuwa anavipeleka.
Serikali tangu mwaka 2007 ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi.