Mkurugenzi wa Utumishi wa (JKT) Kanali Julius Kadawi amesema kuwa nafasi za kujiunga na Jeshi hilo haziuzwi na amewataka vijana kutokubali kutoa fedha zozote ili kujiunga na jeshi hilo huku akisisitiza nafasi hizo zinaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Wilaya na mikoa nchi nzima.
"Zoezi la kuchagua vijana litaanza mapema mwezi Novemba mwaka huu na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT kuanzia Disemba 4, 2017 hadi Disemba 9, 2017. Jeshi la kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi ya kujiunga na JKT haziuzwi na yoyote atakayehusika na kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua"alisisitiza Julius Kadawi
Mbali na hilo Kanali Julius amesema sifa za vijana ambao wanatakiwa kujiunga na jeshi hilo na aina ya vifaa ambavyo vinatakiwa kwa wale ambao watachaguliwa zinapatikana katika tovuti ya JKT.