Spika wa Bunge Job Ndugai amesema hajapokea barua yoyote ya kujiuzulu ya Mbunge wa kaskazini Lazaro Nyalandu mpaka sasa
Spika Ndugai amesema anamtambua mbunge huyo kama mbunge halali kwa kuwa barua yake ya kujiuzulu bado hajaipata
Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha Azam TV Spika Ndugai amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa undani zaidi kwa kuwa hajapokea barua ya kujiuzulu kiongozi huyo na pia amesema ingekuwa vema angempatia barua ya kujiuzulu yeye kwanza kabla ya kutangaza kujiuzulu kwake