Tunafuatilia kwa karibu taarifa ya ajali mbaya sana ambayo imetokea eneo la Changarawe, Mafinga, mkoani Iringa basi la Majinja likitokea Mbeya kwenda Dar es salaam limeangukiwa na kontena na taarifa zisizo rasmi zinasema abiria wengi wamepoteza maisha yao.
Habari hizo pia zinasema hadi sasa kuna maiti 36 hospitalini na ambao wanatibiwa majeraha wodini ni wanne. Tunaendelea kufuatilia.
BREAKING NEWS: WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MAFINGA, IRINGA, LEO BAADA YA BASI LA ABIRIA KUANGUKIWA NA KONTENA
By
Edmo Online
at
Wednesday, March 11, 2015