Polisi waua watuhumiwa watano DSM

Watu watano wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wameuawa katika eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam, katika majibizano ya risasi na Polisi yaliyotokea usiku wa kuamkia leo

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lukula ameeleza kwamba  walipata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna mikakati ya uhalifu imepangwa kufanyika maeneo hayo usiku wa jana, hivyo wakajipanga kwa ajili ya kudhibiti.
Amesema kwamba baada ya muda walioambiwa ulipofika wahalifu hao wengi  ambao idadi yao haikupatikana walifika eneo la tukio na kukutana na polisi kisha kuanza  kupambana.
“Majibizano ya silaha yalikuwa makubwa kwa sababu walikuwa na silaha nzito, lakini Jeshi la Polisi lilijipanga imara kuwadhibiti na kufanikiwa kuwauwa watano na wengine wakatokomea kusikojulikana,” amesema.
Aidha Kamanda wa polisi ameongeza kwamba “Tumejipanga na tunapopata taarifa za uhalifu, pamoja na askari wetu kuwa doria maeneo hayo, lakini hujipanga upya kwa ajili ya kupambana na tukio husika. Wananchi wasiwe na hofu kutoa taarifa kwani jeshi la polisi lipo tayari kulinda raia na mali zao”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo