Mikutano ya hadhara ya siasa kurudi tena

Tume ya Uchaguzi nchini, imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 43, unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, 2017 katika Kata hizo huku kampeni zikitegemewa kuanza Oktoba 27 hadi Novemba 25 mwaka huu.

Kampeni hizo kuelekea uchaguzi wa Kata 43 ambazo zitafanyika kwenye mikoa 9 nchini zinakwenda kufungua mlango wa siasa kwa watu na viongozi mbalimbali kunadi sera zao na ahadi zao kwa wananchi kupitia mikutano ya siasa katika sehemu husika.
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 Rais Magufuli alipiga marufuku mikutano ya siasa na kusema kuwa wakati wa siasa umeisha na sasa ni wakati wa kazi na kuwataka wanasiasa ambao wameshinda kwenye majimbo yao husika ndiyo kufanya mikutano ya kisiasa.   
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo