Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira amethibitisha kukamatwa kwa watu hao watano na kusema sasa wanaendelea kufuatilia watu wengine waliohusika kwenye shambulio hilo na kusema kuwa upelelezi bado unaendelea na pindi utakapokamilika watuhumiwa hao watapelekwa kwenye vyombo vya sheria za hatua nyingine zaidi.
"Ni kweli tumewakamata watu watano ila kwa sasa hatuwezi kuwataja kwa majina kwa kuwa upepelezi bado unaendelea na pindi utakapokamilika basi tutawafikisha mahakamani kwa hatua nyingine za kisheria" alisema Leonce Rwegasira
Aidha Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira amesema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo na matukio mengine mbalimbali ambayo yametokea mkoani Morogoro.
