Bwire amemueleza hayo Rais Magufuli leo, Jumanne alipopata fursa ya kuwasalimu wakazi wa Igogo, wakati wa uzinduzi wa kiwanda.
Kiongozi huyo amelazimika kufunguka hayo ikiwa ni siku moja baada ya Meya huyo aliripotiwa kukamatwa jana na Polisi huku ikidaiwa kuwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella ambapo hata hivyo baadaye aliachiwa huru kwa dhamana.
Hata hivyo, Mongella alikana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza.
Bwire alikamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais Magufuli ambaye yuko ziarani mkoani humo kwa madai ya kutaka kufanya kitu kibaya kwenye msafara wa rais.
Mbali na huyo inadaiwa kwamba tangu Aprili mwaka huu Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro huku kila upande ukituhumu mwingine kuhujumu shughuli za maendeleo.
Jana, Rais Magufuli aliwataka Meya, James Bwire na viongozi wengine wa mkoa huo kumaliza tofauti zao ili wawatumikie wananchi.