Mdee amtahadharisha Nyalandu kuja CHADEMA

Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ndani ya chama chao huku akimtahadharisha  kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa chama hicho

Halima Mdee ametumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha Nyalandu ambaye leo ametangaza kujiuzulu nafasi zake za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na nafasi yake ya ubunge aliokuwa nao.
"Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu".
Mapema leo Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM litangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo