Mbowe amtumia ujumbe Nyalandu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe, amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu

Mwenyekiti Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu. 
"Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu  kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu" ameandika Mh. Mbowe.
Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM mapema leo alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo