Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha (Instagram) Manara ameandika ujumbe wa kumsifia mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi akimfananisha na Cristiano Ronaldo.
Aidha Haji Manara ameenda mbali zaidi na kuhusisha namba ya jezi ya Okwi na idadi ya mabao ambayo Simba itaifunga Yanga kwenye mchezo huo.
“Aliyeshinda tuzo ya FIFA anavaa namba saba, anaeongoza kwa kufunga nchini anavaa namba saba, Emanuel na Ronaldo zina herufi saba, Jumamosi ni siku ya saba ya wiki, tarehe 28 ukiigawa kwa kwa nne (idadi ya herufi za jina la Okwi) unapata saba, nimejipigia hesabu tu, ukibisha kasomee upishi”.
Yanga na Simba zinakutana kwenye raundi ya nane ya Ligi kuu soka Tanzania bara siku ya Jumamosi Oktoba 28 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo.