Mwanahabari Kuhojiwa, Kamati ya Bunge yaonya Polisi

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC imelaani kitendo cha jeshi la polisi mkoani Dodoma kuingilia Muhimili wa bunge kwa kumkamata na kumuhoji kwa zaidi ya saa tatu mwandishi wa habari  Augusta Njoji wa mkoani Dodoma kwa kuripoti habari iliyotolewa na kamati hiyo kuhusu jeshi hilo.

Habari hiyo iliyoripotiwa ilikuwa ikihusu ubadhilifu katika mikataba ya manunuzi magari ya washawasha ambapo jeshi la polisi limehojiwa na kamati hiyo Oktoba 19 mwaka huu, huku kamati hiyo ikiwa tayari imemwandikia barua Spika wabunge ili kutoa muongozo juu ya tukio hilo.
Akisoma tamko la kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nagenjwa Kaboyoka, amesema kitendo kilichofanywa na jeshi hilo ni kukiuka kanuni na taratibu za muhimili huo wa bunge kwani suala la waaandishi kuingia kwenye kamati za bunge lipo katika kanuni za bunge.
"Tunapoona Muhimili mmoja unapoingilia muhimili mwingine kwa nia ya kuficha taarifa ambazo sizo za siri, tunaona kitendo kile ni cha kufanya waandishi wa habari au Kamati ya Bunge ni kulifanya Bunge lisiwe na sauti, kitendo hiki tunakilaani na tunakataa kwamba yoyote mwenye nia ovu ya kutaka kulinyamazisha Bunge au kamati zilizopewa kazi na bunge havitakubalika na tunataka mamlaka husika ichukue hatua kwa kuona kwamba kitendo hicho sicho kitendo halali" 
Mwandishi huyo Augusta Njoji amesema ameshangazwa na tukio hilo kwani yeye alikuwa akitekeleza majukumu yake kama kawaida na hakuwa na kosa lolote.
Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma CPC pia kimelaani tukio hilo na kusema mwandishi huyo hakuwa na kosa ila wanashangazwa na hatua iliyochukuliwa.
Hata hivyo, taarifa zilizotolewa kitengo cha habari cha jeshi la polisi, kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto, amesema kesi hiyo imefutwa kutokana na mwandishi huyo hakuwa na sababu ya kuhojiwa.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo