BAADA ya Malalamiko ya muda mrefu kwa timu ya Azam kutaka kutumia Uwanja wao wa Azam Complex kwa mechi dhidi ya Yanga na Simba hatimaye Bodi ya Ligi ya Shiriukisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limetoa ratiba mpya leo.
Katika ratiba hiyo mpya, Bodi ya Ligi imeweka wazi mechi ya Septemba 9 baina ya Azam dhidi ya Simba itachezwa katika dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi huku Desemba 29 wakiwakaribisha pia mabingwa watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga michezo hiyo yote ikipigwa saa 1 usiku .
Hatua hii inakuja sasa hivi baada ya mara kadhaa Azam kupeleka mapendekezo ya kutaka watumie uwanja wao kwa mechi zote ikiwemo Yanga na Simba ingawa walikuwa wanakataliwa kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wa timu hizo mbili.
Ratiba hiyo iliyotolewa leo ikiwa ni ya marekebisho baada ya ile ya kwanza TFF kuikataa na kuuunda kikosi kazi kwa ajili ya upangaji wa ratiba npya itakayokuwa haina mabadiliko ya ubadilishwaji kila wakati sambamba na kwenda na kalenda ya michezo ya kimataifa ya FIFA.
Maoni ya baadhi ya wadau wa michezo wameonekana kufurahia ratiba hiyo ila wanajua katika kuutumia uwanja huo changamoto mbalimbali zinaweza kujitokeza ila kwa sasa hawawezi kuziona ila mpaka pale kitu kitakapofanyika.