Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Siro amesema katika jeshi la polisi hakuna uteuzi wowote unaofanywa kwa kuzingatia jinsia
IGP Siro ameyasema hayo katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV
Amesema "Mimi huwa siteui makamanda wa polisi kwa kuangalia jinsia, sijui mwanamke au mwanaume, mimi naangalia uwezo huyu mtu nikimteua ataweza? hicho ndicho tunachokiangalia, mambo ya jinsia tuwaachie wanasiasa" amesema IGP Siro