Watoto Mapacha wa Msanii Diamond Platnums Kutoka Burundi hawa hapa

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, wakati sakata la mwanamitindo, Hamisa Mobeto, kuzaa na mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, likiwa bado bichi kabisa na halijafutika akilini mwa watu, mwanamke mwingine kutoka Burundi ameibuka na kudai ana watoto mapacha wa mwanamuziki huyo.
Ishu hiyo imeanzia mitandaoni baada ya mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Jesca, kuposti picha ya Zari anayedai alikuwa shoga ake, na kumshushia kichambo ‘hevi’, huku akimtuhumu kuwa alimpora mwanamuziki huyo, kwani mara ya kwanza alikuwa ni wake na yeye alikuwa akimuita shemeji.
Baada ya kumchamba Zari, akaposti tena picha yake akiwa na watoto wake mapacha anaodai kuzaa na mzazimwenziye Zari, akimuomba aje awachukue watoto wake.
Mpaka sasa bado mwanamuziki huyo ambaye ni baba watatu kwa sasa, hajathibitisha kuwa anamfahamu mwanamke huyo na hao watoto ni wa kwake kweli.
NA ISRI MOHAMED/GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo